South Africa: Julius Malema ataka Kiswahili kiwe lugha moja Afrika nzima

Kiongozi wa chama cha watetezi wa Uhuru wa kiuchumi (EFF) cha Afrika Kusini, Julius Malema, ametoa wito wa kupitishwa kwa lugha moja itakayotumika barani Afrika, huku akipendekeza lugha ya Kiswahili kuwa lugha hiyo.

Malema aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na EFF, ambapo aliongelewa mambo mbalimbali ikiwemo ujumbe wa Rais wa Marekani kwenye mtandao wa Twitter kuhusu marekebisho ya sheria ya ardhi Afrika Kusini.

"Tunatakiwa kuzalisha lugha moja ambayo itatumika kwenye bara zima. Kwa mfano Kiswahili, kinaweza kukuzwa ili kitumike barani kote" alisema Malema.

Lugha ya kiswahili ni lugha inayotumika sana barani Afrika, ambapo kinatumika sana Afrika mashariki na kati. Ni lugha rasmi kwa nchi ya Tanzania na Kenya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad