Steve Nyerere Amshukuru Faiza Alli Baada ya Kumtetea "Wewe ni Original Ulembi"

Steve Nyerere Amshukuru Faiza Alli Baada ya Kumtetea "Wewe ni Original Ulembi"
Kumekuwa na tetesi kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na Steve Nyerere ambapo wengi wamedai kuwa amekuwa mtu wa kuhudhuria misiba na kuchukua michango inayotolewa kwenye misiba anayohudhuria kutokana na kujivika bendera ya uongozi.

Kupitia mitandao ya kijamii baadhi ya waigizaji wameonekana kuguswa na maneno yanayoendelea kumuandamana Steve Nyerere kwenye mitandao ya kijamii kwa tuhuma mbalimbali,  Muigizaji Faiza Ally aliamua kufunguka na kumtetea Steve Nyerere kwa kile anachoamini anavunjiwa heshima.

 “Nimefikiria jambo hili kwa muda na nimeona nilazima nijiridhishe kwa kusema haya @stevenyerere2 amekua akichekwa na kudharaulika halafu wasanii wamekaa kimya ni kama vile hawajui umuhimu wa uwepo wake , kiukweli sijaona mwanaume bongo movie mwenye uwezo wa kusimamia chochote kama anavyo simamia Steve pindi linapotokea jambo la wito na si msiba peke yake !“

“Ni nani anaweza kusimama na si kusimama tu na kutafuta hela na michongo ?????? Na of course bongo movie ni kitu kikubwa kinahitaji mtu kama Steve ni muhimu na nafasi yake ni kipekee inatakiwa iheshimike na zaidi anahitajika …sasa anapopata kashfa na mnakaa kimya zaidi mnamcheka ni sawa hivyo? Wangapi amewasaidia kupata dili za kampeni ? Wangapi amewaombea michango ya matibabu ? Wangapi amewapa connection za hela?”

“Misiba mingapi amesimama nani angefanya ?????? na mpaka sasa anachekwa anatengenezea vikatuni vya dharau wote mko kimya …kwa nini msisimame na kukanusha shutuma anazopata ??? Hali yakuwa mnajua wengi wenu maskini na mnamuhitaji ??? Ndio atakua bora pale msaada wake unapo hitajika?”



Baada ya post hiyo Steve Nyerere alimshukuru Faiza Ally kupitia ukurasa wake wa instagram kwa kugundua kile ambacho kinaendelea kwenye mitandao ya kijamii

“Nimeangalia ulicho andika nikagundua upo tofauti na viumbe wengine yani wewe ni original ulembi hahahaha asante shemeji yangu na tupo pamoja sana kwenye shida na raha”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad