Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye amesema moja ya dalili za chama cha siasa kilichochokwa na wananchi ni kutumia nguvu.
Sumaye ambaye ni mwenyekiti wa Chadema kanda ya Pwani ametoa kauli hiyo jana Alhamisi Agosti 30, 2018 wakati akimnadi mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Ukonga, Asia Msangi katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Gulu Kwalala.
Alisema CCM imechokwa na wananchi na kwa saa inachokifanya ni kung’ang’ania madarakani kwa kutumia nguvu.
“Kama unajiamini na wananchi wanakukubali kwa nini uwaonee wananchi, uwatishe kwa kila aina ya vitisho. Huko ni kujilazimisha kuwa wananchi wanakukubali wakati unawaziba midomo. Unawalazimisha kukubali unachokitaka,” alisema.
Amesema wanaopenda mabadiliko ndani ya Chadema, CUF na hata CCM, huu ndio wakati wao wa kujipambanua na kuonyesha uwezo wao katika siasa kwa kufanya uamuzi sahihi.
“Hivi kweli hatuna akili kiasi hiki? Mtu tulimpa kura hapa hapa na ametutukana hadharani na bado tunampa tena” alihoji Sumaye akimlenga mgombea wa CCM katika jimbo hilo, Mwita Waitara , ambaye awali alikuwa mbunge wa Ukonga kwa tiketi ya Chadema.
Hoja yake haina msingi maana haikuzingatia ukweli uliopo.
ReplyDeleteUsirudieKosaKupigiaKuraUpinzaniOvyoo!