Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania TFF limemtangaza rasmi nyota wa zamani wa timu ya Taifa Nigeria na klabu ya Barcelona, Emmanuel Amunike kuwa kocha mkuu wa Taifa Stars kwa mkataba wa miaka miwili.
Anakumbukwa zaidi kwa mabao yake mawili aliyofunga katika fainali za kombe la dunia kule nchini Marekani, Amunike ameshinda vikombe kadhaa akiwa kama mchezaji katika nchi za Nigeria na Egypt, alipokuwa akiichezea Julius Berger F.C. na Zamalek SC.
Mwaka 1994, alijiunga na Sporting Clube de Portugal, na alifanikiwa kufunga mabao 7 kwenye msimu wake wa kwanza bila kusahau bao muhimu alilowafunga S.L. Benfica kwenye dabi ya Lisbon (1–0 na kuwapa Sporting ubingwa wa kombe la Ureno mnamo mwaka 1994)
Mwaka 1996 mwezi wa 12 Amunike alinunuliwa na klabua ya La Liga FC Barcelona kwa ada ya $3.6 millioni. Aliichezea Barcelona mechi tatu za msimu wa kwanza baada ya kuumia goti.
Amunike aliteseka sana na goti lake mpaka pale Barça ilipomuuza mwwka 2000, na akaelekea Albacete Balompié (ya nchini Hispania iliyokuwa ligi daraja la kwanza Segunda División). Alistaafu soka akiwa na umri wa miaka 34 . Mwaka 2008, alikwenda ligi kuu Saudi kwenye klabu ya Al-Hazm akiwa anafanya kazi kama kocha msaidizi kabla hajawa skauti wa klabu kubwa duniani Manchester United.