Tanzania Hakuna Upinzani- Cheyo

Tanzania Hakuna Upinzani- Cheyo
Mwenyekiti wa chama cha siasa cha UDP Taifa John Cheyo amefafanua kuwa Tanzania hakuna chama kilichosajiliwa kuwa upinzani bali ni sera na Katiba itakayokiongoza huku lengo likiwa ni kuanzisha chama cha siasa kwa ajili ya ushindani wa hoja za maendeleo kwa wananchi.

Cheyo amesema hayo kwenye kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio ambapo amebainisha kuwa siasa sio uadui na ndio maana hata yeye alipatiwa nafasi ya kwenda kumuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli nchini Zimbabwe kwenye sherehe za kuapishwa kwa rais wa pili wa taifa hilo.

“Tunachokosea ni kuanza siasa za chuki wakati hilo sio lengo la mfumo wa vyama vingi, tujifunze kupitia rais wetu Dkt. Magufuli kauli zake za kila siku kuwa ni rais wa Watanzania wote na kusisitiza kuwa maendeleo hayana chama,” amesema Cheyo ambaye ni maarufu kwa jina la Bwana Mapesa.

Rais Dkt. John Magufuli alimuomba Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete kumwakilisha katika sherehe za uapisho wa Rais mteule wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa zilizofanyika Agosti 26, Jijini Harare ambaye alifatana na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (Bara), Philip Japhet Mangula pamoja na Mwenyekiti wa chama cha UDP Cheyo.

Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza tangu kiongozi wa muda mrefu wa nchi ya Zimbabwe, Robert Mugabe, kung'olewa madarakani na kupelekea kuibua hisia kali za kisiasa nchini humo kwa kile kilichoonekana watu kuchoshwa na tawala za mabavu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad