Shirika la viwango nchini TBS limebaini kuwepo kwa nyaya na vifaa vingine vya kupitishia umeme vinavyouzwa kwenye maduka kariakoo huku vifaa hivyo vikiwa havina ubora.
Mratibu wa ukaguzi huo, Simon Emmanuel na Afisa Udhibiti Ubora, Daudi Nkugile wamesema shirika hilo litalazimika kuteketeza vifaa hivyo kwa gharama za wenye mali ili iwe fundisho kwa wafanyabiashara wenye tabia ya kuingiza sokoni bidhaa zisiso na viwango au zenye viwango hafifu.
Wakizungumza wakati wa zoezi la ukaguzi wa bidhaa mbali mbali kwenye maduka yaliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam, maafisa wa TBS wamesema vifaa vilivyokamatwa ni hatari kwa usalama wa majengo na maisha ya watumiaji.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage wakati akisoma bajeti ya wizara yake Bungeni mjini Dodoma, alisema kuwa watumishi wa umma watakaoruhusu bidhaa feki Julai mosi mwaka huu, kuingia kwenye soko la ndani wajiandae kuachia nafasi zao.