TFF Yaungana na Makonda Katika Maandalizi wa AFCONU17

TFF Yaungana na Makonda Katika Maandalizi wa AFCONU17
Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), kupitia kwa Rais wake Wallace Karia, limethibitisha kupata ushirikiano kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam katika maandalizi ya michuano ya kuwania kufuzu AFCON U17 mwaka 2019 kwa vijana kutokea katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.


Rais wa TFF Wallace Karia (kushoto) na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda (kulia).

Karia amebainisha hilo leo kwenye mkutano wa pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda, TFF na wanahabari, ambapo amesema taratibu zote za mapokezi ya timu kutoka mataifa 12 zinaratibiwa kwa pamoja na ofisi ya mkoa pamoja na shirikisho na kila kitu kipo sawa.

''Kwa upande wetu maandalizi ya michuano hiyo itakayoanza Agosti 11 kwa kushirikisha timu 12, yameshakamilika ila tu tuishukuru serikali ya mkoa wa Dar es salaam kwa ushirikiano wanaotupatia kwenye mapokezi na usalama wa timu'' - amesema.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda, amesema wamejipanga kama mkoa kuhakikisha michuano hiyo inafanyika kwa mafanikio ili kurejesha imani kwa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) na kusaidia kuendelea kupewa fursa ya kuandaa mashindano mengine.

Michuano hiyo ya vijana ambapo Tanzania tayari imefuzu fainali za mwakani kwa kigezo cha kuwa mwenyeji, inaanza Agosti 11 na kumalizika Agosti 26. Timu zitakuwa kwenye makundi mawili na zitacheza kwa mfumo wa ligi na baadae robo fainali, nusu na fainali. Bingwa atapata nafasi ya kuwakilisha Ukanda wa CECAFA kwenye AFCON U17 ya 2019

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad