TID Awatungia Wimbo Basata

TID Awatungia Wimbo Basata
Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Khaleed Mohamed ‘TID’, amesema hawezi kupeleka kazi zake kukaguliwa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), kwa madai yeye ni miongoni mwa wanamuziki waliosajiliwa na baraza hilo.

TID amebainisha hayo alipokuwa anazungumza kwenye heshima ya bongo fleva iliyopo ndani ya kipindi cha PLANET BONGO kinachorushwa na East Africa Radio, muda mchache alipomaliza kutambulisha ngoma yake mpya ya 'washa' yenye miondoko ya mduara aliyomshirikisha mwanamuziki Kassim Mganga.

"Hii ngoma BASATA sijaipeleka lakini mimi ni msanii niliyesajiliwa na BASATA, na haki zangu zote zipo COSOTA kwa hivyo BASATA wananifahamu sana kwa vibao vyangu murua na matata. Kibao kama hichi BASATA hawana hata haja ya ku-preview na kwa heshima waliyokuwa nayo BASATA, kibao hiki nimewatengenezea wao", amesema TID.

Mbali na hilo, TID amekanusha zile tetesi zilizokuwa zikisambaa mitandaoni kuwa alivunja mabango ya BASATA na kutokana walimzingua kwa namna ama nyingine na kudai sio kweli bali muziki ndio ulikuwa umemzingua na wala sio BASATA.

Katika miaka ya hivi karibuni Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), lilitoa kanuni zake mpya ambazo zilikuwa zinawataka wasanii kupeleka kazi zao zikaguliwe kabla hazijawafikia mashabiki, kwa lengo la kuangalia maudhui yaliyotumika pamoja na suala zima la maadili kama wamezingatia.
TAZAMA VIDEO MPYA YA ROSA REE HAPA CHINI ALIYOTOA LEO..
HAYO MAUNO SI YA NCHI HII:



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad