Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemkuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa (TBC) Tido Mhando katika kesi yake ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh.Mil 887.1 ambapo ataanza kujitetea September 20 2018.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai kufunga ushahidi wa mashahidi 5 wa upande wa mashtaka.
Hakimu Shaidi amesema amepitia ushahidi wote wa mashahidi watano ulioletwa na upande wa mashtaka na kuona mshtakiwa ana kesi ya kujibu, ambapo ameahirisha kesi hadi September 20 2018 ili Tido aanze kujitetea.
Katika kesi hiyo Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.Milioni 887.1 na miongoni mwa mashahidi wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi ni Ofisa uchunguzi wa Takukuru Victor Lesuya Mwanasheria wa TBC Gwakisa Mlawa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC Clement Mshana.
Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa June 16, 2008 Mbando akiwa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido ambaye alikuwa mkurugenzi wa TBC kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.
Tido Mhando Akutwa na Kesi ya Kujibu Atakiwa Kujitetea Septemba 20
0
August 27, 2018
Tags