Timu ya taifa ya wanawake ya Japan chini ya miaka 20 (U20) imeibuka bingwa katika michuano ya kombe la dunia kwa timu za wanawake chini ya miaka 20 iliyofanyika nchini Ufaransa baada ya kuifunga Hispania kwa goli 3-1.
Nafasi ya tatu imechukuliwa na timu ya taifa ya Uingereza walioifunga Ufaransa kwa penalti 4-2 baada ya dakika 120 za mchezo huo kumalizika kwa kufungana bao 1-1.
Michuano hii ilianza kutimua vumbi Agosti 5 mpaka Agosti 24 mwaka huu ilishirikisha timu 16 huku bara la Afrika likiwakilishwa na timu mbili za nNigeria na Ghana.
Ghana iliishia hatua za makundi na Nigeria ilifika robo fainali na kutolewa na Hispania kwa magoli 2-1.
Mbali na kuibuka mabingwa Japan pia wametwaa tuzo ya Uchezaji wa Haki "Fair Play".