Trump Atishia Kuichukulia Hatua Mitandao ya Google, Twitter na Facebook kwa Kuminya Taarifa Zake

Trump atishia kuichukulia hatua mitandao ya Google, Twitter na Facebook kwa kuminya taarifa zake
Rais wa Marekani Donald Trump amezionya kampuni za mawasiliano ya mtandao Google, Twitter na Facebook kwa kile alichokiita kuminya taarifa zake na za mrengo wa kihafidhina.

Trump ameitaka mitandao hiyo kuwa makini baada ya awali kuishutumu Google kwa kupindua matokeo ya taarifa pale mtumiaji wa mtandao huo anapotafuta habari kumhusu Trump.

Hata hivyo, Google wamekanusha shutuma kuwa mtandao wao unaupendeleo na kusema hawafungamani na itikadi yoyote ya kisiasa.

Akiongea na wanahabari katika ikulu ya White House, Trump amesema, "Google wamekuwa wakihadaa watu wengi, ni jambo zito sana."

Akaziongeza pia kata lawama Twitter na Facebook, "inawapasa wawe makini, hauwezi ukawafanyia watu mambo haya…tunapokea maelfu ya malalamiko juu ya jambo hili."

Rais Trump hatahivyo hajabainisha ni hatua gani hasa ambazo utawala wake unapanga kuzichukua.

Awali mshauri wa Trump wa masuala ya uchumi, Larry Kudlow amesema utawala kwa sasa unaangalia ni namna gani wataliendea suala hilo kwa kuangalia kanuni za udhibiti.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad