Trump Azikana Tuhuma za Kutumia Fedha Wakati wa Kampeni Kuwalipa Wanawake Ili Kuwanyamazisha

Trump Azikana Tuhuma za Kutumia Fedha Wakati wa Kampeni Kuwalipa Wanawake Wawili Ili Kuwanyamazisha
Rais wa Marekani amekana vikali tuhuma za kuhusika kwake katika kutumia fedha wakati wa mikutano ya kampeni kuwalipa wanawake wawili ambao wanasadikiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye.

Katika kesi iliyosikilizwa katika mahakama moja mjini New York mapema wiki hii , mwanasheria wa zamani wa rais Trump, Michael Cohen, amesema kuwa Trump alimpa maelekezo kutoa fedha kwa lengo kuu la kuwashawishi wanawake hao kukaa kimya wakati wa uchaguzi wa rais wa 2016.

Ingawa katika mahojiano na kituo cha runinga cha Fox News, Raisi Trump alitoa ufafanuzi kuwa malipo hayo yalitoka katika fedha zake binafsi na hazikuwa fedha za kampeni kama inavyodhaniwa.

Na kuarifu kuwa alikuja kutanabahi juu ya malipo hayo baadaye, ingawa hakubainisha kuwa miamala hiyo ilifanyika wakati gani.

Raisi Trump amekuwa akimshutumu bwana Cohen kwa kupika mambo dhidi yake kwa lengo la kupata huruma na kuepuka kifungo.

Ikulu ya white house, imesisitiza kuwa kuvunja sheria ya fedha za kampeni kwa Michael Cohen hakumaanishi kuwa basi Rais trump naye atawajibika, msemaji wa white house sarah sanders amekataa kusema ni lini Rais Trump alijua juu ya malipo ya wacheza filamu wawili wa ngono

''kama rais alivyosema katika matukio tofauti tofauti, hajafanya kitu chochote kibaya, hakukua na madai yoyote dhidi yake katika hili, na kwasababu tuu Michael Cohen amekiri makossa yake haimaanishi inamgusa rais''

Katika kukiri makosa yake siku ya jumanne bwana Cohen alisema kuwa ametumwa na Trump kufanya malipo hayo lakini white house imekataa madai haya.

Malipo yafanywayo kwa siri kwa niaba ya mwanasiasa ama mgombea yeyote yanaweza kuchukuliwa kama ukiukwaji wa sheria za kampeni za nchini Marekani
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad