Trump: Mazoezi ya Kijeshi na Korea Kusini Yatakuwa Makubwa Zaidi

Trump: Mazoezi ya kijeshi na Korea Kusini yatakuwa makubwa zaidi
Rais wa Marekani Donald Trump ameikosoa China kwa kuhujumu jitihada zake na Korea Kaskazini, wakati kuna malalamiko kuhusu maendeleo ya kuharibu silaha za nyuklia za Korea Kaskazini.

Kupitia ujumbe wa Twitter alisema hakuna sababu ya kutoendelea tena na mazoezi ya kijeshi na Korea Kusini ambayo yamekuwa yakiikasirisha Korea Kaskazini.

Siku zilizopita waziri wake wa ulinzi alisema mazoezi ya kijeshi yanaweza kuendelea.

China imeikosoa Marekani kwa kuilaumu kuhusu uhusiano wake na Korea Kaskazini.

Taarifa za vitisho vya kivita kati ya Marekani na Korea Kaskazini 2017
Mkutano kati ya Bw Trump na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un mwezi Juni ulikamilika kwa ahadi kutoka Korea Kaskazini kufanya kazi katika kuharibu silaha za nyuklia kwenye rasi na Korea.

Baadaye Trump alitangaza kuwa hakukuwa tena na tisho kutoka Korea Kaskazini.

Lakini tangu wakati huo waangalizi wengi wanasema kuwa Korea Kaskazini haifanyi hima katika kuharibu maeneo yake ya kurushia makombora.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad