Tumeuzika muziki wetu"- Z Anton

Msanii mkongwe wa bongo fleva, Z Anton amefunguka na kudai sababu kubwa ya muziki nchini Tanzania kutofanya vizuri, ni kutokana na wasanii wakubwa kutengeneza 'kiki' sizizokuwa na msingi na mwisho wa siku wanatoa nyimbo ambazo hazifananii na walichokitengeneza.


Msanii mkongwe wa bongo fleva, Z Anton

Z Anton amebainisha hato wakati alipokuwa anazungumza na www.eatv.tv baada ya kuwepo wimbi kubwa la wasanii wa bongo fleva hata wale wa upande wa pili kupendelea kufanya hivyo, na kupelekea soko la muziki kushuka nchini kutokana na vitendo kama hivyo.

"Msanii ambaye anafanya 'kiki' ni mtu hajiamini kwasababu ukiwa na ngoma kali, utakuwa na sababu gani za kufanya 'kiki'. Tumeuzika muziki wetu kwasababu kama hizi maana utakuta watu wanatengeneza tukio kubwa halafu ukija kusikiliza nyimbo unakuta ya kawaida tu, mwisho wa siku ukifanya jambo lolote watu wanakupuuza", amesema Z Anton.

Pamoja na hayo, Z Anton ameendelea kwa kusema kuwa "umaarufu waliokuwa nao wasanii wa sasa sio wa kutisha sana kutokana na 'kiki' zao ambazo wanazifanya, ila kilichowasaidia ni kutokana na 'game' kuwa limetanuka ndani na nje ya nchi, lakini hakuna star ambaye aseme akae kimya kwa miezi sita au mwaka halafu aendelee kujulikana".

Mbali na hilo Z Anto amesema ukimya wake katika muziki ulitokana na yeye kuwa 'busy' na biashara zake binafsi, pamoja na kusoma mapungufu ya wasanii wa sasa huku akidai kwamba hatashindwa katika mashambulizi ambayo ameyandaa pindi atakaporudi kwa mara nyingine.

"Ukimya wangu katika biashara umetokana na u-busy wa biashara zangu ninazozifanya pamoja na maandalizi yangu ya kurudi kwa mara nyingine, katika 'game' kwa kuwa nilikuwa nataka kila 'audio' iwe na video yake kabisa. Na katika hilo hadi dakika hii nimeshatimiza kwa asilimia 80 kwa baadhi ya plan ambazo nilizokuwa nazo, kwa hiyo najiamini nipo katika mazingira magumu wakati huu", amesisitiza Z Anton.

Kwa mara ya mwisho sauti ya Z Anton iliweza kusikika katika wimbo wake wa 'wake up Tundu Lissu' aliouachia Septemba 11 mwaka 2017, ambao ulikuwa unazungumzia juu ya tukio la mwanasiasa huyo kupigwa risasi na watu wasiojulikana mnamo Septemba 7 mwaka huo huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad