Hello Friends of Me!!!
Good afternoon to y'all. Kwa mara nyingine nawaleteeni habari njema.
Alfajiri ya tarehe 6 January ya mwaka huu, niliondoka Nairobi Hospital na kusafiri hadi Leuven, Ubelgiji, kwa ajili ya matibabu zaidi. Jana tarehe 6 Agosti ilikuwa mwezi wa saba kamili tangu niletwe hapa Ubelgiji kwa ajili hiyo.
Leo tarehe 7 Agosti ni miezi 11 to the day niliposhambuliwa na watu wanaojulikana sana kama 'watu wasiojulikana.'
Tarehe 7 September mwaka jana sikulala nyumbani kwangu. Tarehe 7 Agosti ya leo, miezi 11 kamili baadae, nimeamkia nyumbani kwangu.
Tarehe 7 September iliyopita wote mlikuwa na hofu kubwa kama ningemaliza siku hiyo, au siku chache zilizofuata, nikiwa hai. Miezi 11 kamili baadae, Professor Dr. Wilhelmus Jan Mertsemakers, daktari wangu tangu nilipokuja University Hospital Leuven, amesema sina sababu ya kitabibu ya kuendelea kukaa hospitali.
Prof. Mertsemakers amesema nitaendelea na uponyaji nikiwa nyumbani kwangu. Nitatembelewa na homecare nurses kila siku nyumbani kuniangalia naendeleaje. Na nitarudi hospitali kumwona kila baada ya wiki mbili.
Bado nina lichuma kubwa kwenye paja liko kama antenna ya TV za mwaka '47. Na Prof. Mertsemakers amesema nitakaa nalo kwa si chini ya miezi sita. Lakini habari ya mujini ndio hiyo: nimetoka hospitalini.
Hongereni sana kwa kazi nzuri ya kuniuguza na kuniponya. Na chochote mtakachokula au kunywa siku ya leo mnibakishie. Siko mbali.
Tundu Lissu,
Brussels, Belgium.