Uchaguzi Zimbabwe: Jamii ya Kimataifa Yatoa Wito kwa Zimbabwe Kukomesha Ghasia

Uchaguzi Zimbabwe: Jamii ya Kimataifa Yatoa Wito kwa Zimbabwe Kukomesha Ghasia
Matumizi ya nguvu ya serikali dhidi ya upinzani nchini Zibabwe baada ya uchaguzi wa Jumatatu yameichochea jamii ya kimataifa kutoa wito wa kumaliza vurugu.

Umoja wa mataifa na umoja wa ulaya kwa pamoja wamekemea juu vurugu zilizotokea na polisi kufyatua risasi kwa waandamanaji.

Makundi ya waandamanaji yalikuwa katikati ya mji huo tangu alfajiri lakini habari zilipozuka kwamba Zanu PF imeshinda viti vingi katika bunge na kwamba matokeo ya urais hayakuwa tayari , hali ilibadilika.

Uchaguzi wa Jumatatu ulivutia asilimia 70 ya wapiga kura. Chombo cha habari cha ZBC kimesema kuwa Zec itatangaza matokeo ya uchaguzi wa urais mwendo wa 12.30 za Zimbabwe.

Tume ya uchaguzi nchini Zimbabwe inasema asilimia 70 ya wazimbabwe walijiandikisha kupiga kura
.Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amesema kuwa serikali ya Zimbabwe inatakiwa kuhkikisha kuwa vurugu hizo hazitokei.

Wakati huo huo shirika la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International linaitaka serikali kufungua mashataka kwa polisi waliofyatua risasi kwa waandamanaji.

''vikosi vya usalama vinapoingilia uchaguzi ni kuwanyima haki wananchi ya kujieleza'' amesema katibu wa Amnesty.

Tume ya uchaguzi ya Zimbabwe(Zec) hadi sasa imetangaza ushindi wa viti 140 kwa chama tawala cha Zanu-PF, huku kile cha Muungano wa Upinzani MDC kikiwa na viti 58 , Kulingana na taarifa ya Shirika la Utangazaji la taifa ZBC . Kuna viti 210 Katika Bunge la Taifa la taifa.

Zaidi ya watu milioni tano walijiandikisha kupiga kura, na watu wengi walijitokeza kushiriki uchaguzi kwa kiwango cha 70%.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad