Mwenyekiti wa kamati ya usajili na mashindano Yanga, Hussein Nyika amefafanua kwa nini kocha Zahera Mwinyi hakai kwenye benchi kutokana na kukosa kibali cha kufanyia kazi licha ya muda mrefu kupita tangu kocha huyo kusaini mkataba wa kuifundisha Yanga.
“Wanayanaga wanatakiwa wajue sio Yanga inayotoa kibali, ni taratibu za kiserikali zinajulikana na bahati mbaya au nzuri watu wote wanajua makao makuu ya nchi yamehamia Dodoma kwa hiyo michakato ya kwenda Dodoma kufatilia vibali na hapa katikati kulikuwa na bunge la bajeti kwa hiyo wizara ilikuwa na mambo mengi sana.”
“Kibali kimepatikana Alhamisi lakini kilikuja kwa kuchelewa kwa hiyo kufuatilia uhamiaji Ijumaa tukawa tumechelewa ndio maana Jumamosi hakuweza kukaa kwenye benchi.”
“Kibali nimekithibitisha mwenyewe jana (Jumatatu) nina hakika mechi ijayo mwalimu atakaa kwenye benchi.”