United wanajiandaa kumfukuza Mourinho?

Hizi ni tetesi lakini zinaonekana zina ukubwa sana, Jose Mourinho ni moja ya makocha ambao wanapewa nafasi kubwa sana kutimuliwa msimu huu wa ligi kama hatafanya vizuri.

Na sio utani United hawataki kuburuzwa tena hawako tayari kuona timu kama Manchester City au Chelsea wanachukua tu kombe mbele yao kila kukicha huku wao United wanabaki kama wasindikizaji.



Lakini kitendo cha Manchester United kumtimua Jose Mourinho(kama wakifanya hivyo) baasi itawagharimu kiasi kikubwa sana cha fedha.

Manchester United watahitajika kulipa kiaso cha £12m kwa kocha huyo wa Kireno ambapo kiasi hicho ni sawa na mshahara wake wa mwaka mzima na haijalishi atatimuliwa mda gani bali pesa hiyo anapswa kupewa.

Jose Mourinho alisaini mkataba mpya na United utakaomuweka hadi mwaka 2020 lakini klabu hiyo ili kuogopa hasara waliamua kuweka kipengele katika mkataba wake ambacho hawatampa pesa yote ya mkataba wake kama utaishia katikati.



Tangu ajiunge na Manchester United Jose Mourinho ameshacheza mechi 120 huku kati ya hizo akishinda michezo 74 suluhu 25 na amefungwa michezo 21.

Manchester United ni klabu ambayo haitaki makombe madogo dogo na target kubwa ya klabu imekuwa makombe makubwa kama Championd League na Epl ambayo hawajawahi yapata toka Fergie aondoke huku pesa wanayotumia ya usajili ikiwa kubwa.

Orodha ya Makocha na pesa walizotumia tangu Ferguson aondoke.

David Moyes. Moyes ndiye alikuwa mrithi wa Fergie United na alipojiunga tu alipewa pesa akamnunua Marouane Fellaini kwa £27.5 kutokea Everton kisha Juan Mata kutoka Chelsea.



Louis Van Gaal. Baada ya Moyes mikoba ikaenda kwa Van Gaal ambaye aliwanunua Ander Herrera £32.4m kutoka A Bilbao, Luke Shaw £27m kutoka Southampton, Marcos Rojo £16m kutoka Sporting, Angel Di Maria £60m kutoka Real Madrid, Daley Blind £14m kutoka Ajax na kwa ujumla alitumbua £149m.



Msimu wa 2015/2016 akamnunua Depay kwa £25m(Psv Endhoven), Matteo Darmian £12.7m(Torino), Bastian Schweinsteiger £6.5m, Morgan Schnedelin £25m(Southampton), Anthony Martial £58m(Monaco).

Jose Mourinho. Baada ya LVG kutimuliwa ndipo Mourinho akachukua mikoba yake akaanza na Eric Bailly £30m(Villareal), Ibrahimovich free(PSG), Henrikh Mkhitaryan £27m(Borussia Dortmund), Paul Pogna £89m(Juventus) jumla £146m.



Msimu wa 2017/2018 akamnunua Romelu Lukaku £75m (Everton), Victor Lindelof £30(Benfica), Nemanja Matic £35m(Chelsea), jumla hapa akatumia £140m na hadi sasa ameshamnunua Fred

Kwa ujumla makocha hawa watatu wametumia kiasi cha zaidi ya £600m tangu Ferguson aondoke na hii inawafanya United kutokuwa na huruma pale kocha akishindwa kuwapa wanachotaka.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad