United Yakanusha ujio wa Zidane ‘Kwa nini Tumzungumzie Wakati Hakuna Nafasi ya kazi’


Klabu ya Manchester United imesisitiza kuwa haijawahi kufanya mawasiliano yoyote na aliyekuwa meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane ili kuja kuchukua nafasi ya Jose Mourinho Old Trafford kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Baadhi ya wadau wa soka wamekuwa wakimtabiria mabaya Mourinho kuwa ndiye meneja wa kwanza ligi kuu Uingereza atakayetimuliwa kutokana na matokeo mabaya ambayo amekuwa akiyapata hata kipigo cha mabao 3 – 2 dhidi ya Brighton.


 Chombo kimoja cha habari nchini Ufaransa ndicho kilichoanza kuripoti kuwa Zidane mwenye umri wa miaka 46 ameonyeshania kutua United kurithi mikoba ya Mourinho baada ya kupata mafanikio ya kutwaa mataji matatu ya  Champions League mfululizo.

Chanzo cha ndani kutoka United kimesisitiza kuwa Mourinho bado ataendelea kusalia huku akishindwa kukubali kuwa na mazungumzo na Zidane kwa kusema ”Kwa nini tumzungumzie yeye wakati hakuna nafasi ya kazi.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad