Uswizi Watakiwa Kuwavalisha Mbwa Wao Viatu


Uswizi Watakiwa Kuwavalisha Mbwa Wao Viatu
Polisi kwenye mji wa Uswisi wa Zurich wanawashauri watu kuwanunulia mbwa wao viatu ili kuwakinga kutokana na athari za viwango wa juu vya joto.

Kulingana na kituo cha habari cha kitaifa SRF, polisi mjini Zurich wamezindua kampeni ya kuwapa ushauri wamiliki wa mbwa, jinsi wanaweza kuwakinga kutokana na joto la juu, kutokana na sababu kuwa veranda zinaweza kuwa zenye joto.

Kipindi cha joto la juu barani Ulaya inamaana kuwa Uswizi ina msimu ya juu ya joto tangu mwaka 1864 huku viwango vya joto vya mwezi Julai vikifikia nyuzi 30.

"Wakati mbwa anatembea eneo lenye moto anaweza kuchomeka miguu sawa na binadamu anayetembea bila viatu."

Polisi kwenye mji wa Zurich sasa wanawashauri wenye mbwa kufanya ukaguzi kabla ya kuwapeleka mbwa wao nje kwa kutumia mkono wao kwa sekunde tano.

Pia wamewashauri wale wanaowatunza wanyama kutowaacha kwenye magari yao na wahakikishe kuwa wana maji ya kutosha ya kunywa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad