Mchungaji wa kanisa la Full Gospel Tabernacle in Jesus, Cody Coots amejikuta akiupigania uhai wake baada ya kung’atwa na nyoka wakati akishusha maombi mbele ya waumini wake.
Cody Coots ameng’atwa na nyoka huyo ndani ya kanisa lake lililopo Middlesboro, Kentucky nchini Marekani licha ya kutambua kuwa amejeruhiwa na damu zinatoka mchungaji huyo aliendelea na ibada kama kawaida bila kujali ndipo akajikuta akiishiwa nguvu na kupata msaada kutoka kwa wasaidizi wake.
Kwa mujibu wa tovuti ya Mirror na baadhi ya mitandao mbalimbali imesema kuwa mchungaji huyo baada ya kung’atwa na nyoka wakati akitoa huduma hiyo alisikika akipiga kelele akisema kuwa Mungu ni mponyaji na hakubaliani na nyoka.
Kipande cha video kilichoenea kwenye mitandao mbalimbali kinaonyesha namna alivyokuwa akifanya ibada hiyo na mpaka tukio la kung’atwa likatokea. Huku mchungaji Cody akiomba kupelekwa kwenye kilele cha mlima mbapo Mungu ataamua uhai wake wa kuishi ama kufa.
Kanisa hilo lilishawahi kumpoteza mchungaji wake, Jamie Coots ambaye alikuwa baba wa kiongozi huyu wadini Cody Coots baada na yeye kung’atwa na kufariki mwaka 2014 akiwa na umri wa miaka 60.
Habari hiyo ya hapo kanisani imepewa jina la My Life Inside: The Snake Church, baada ya kipande cha kwanza cha filamu kurushwa na Barcroft TV.
Kifo cha baba yake kilimfanya Cody kuingia kwenye majukumu hayo ya uchungaji akiwa na umri wa miaka 23 pekee ambaye na yeye ameng’atwa na nyoka na kwa sasa akiwa hopsitalini kwa matibabu zaidi.
Vifo vinavyosababishwa na nyoka katika kanisa hilo vimekuwa vya kawaida baada ya baba yake na Cody ambaye ni mchungaji, Jamie Coots kuuwawa na nyoka mwaka 2014, David Brock naye akifariki mwaka 2015 kwa kinjia hiyo hiyo ya kung’atwa na nyoka akiwa na miaka 44, Mack Randall Wolford akiumwa na nyoka na yeye kando ya kanisa hisa mwaka 2012.
Wakati mke wa mchungaji huyo, Tammy mwenye umri wa miaka 25 akisema kuwa kanisa hilo limejaa damu yao kutokana na familia kuwa waathirika wa kubwa tangu zama za baba mzazi wa mchungaji huyo, Jamie Coots aliyengatwa na nyoka.