Video: Ommy Dimpoz Afunguka Kuhusu Ugonjwa ‘Kuna Hospitali Bongo iliniambia hii ni Kansa,

Msanii wa muziki Ommy Dimpoz ambaye anaumwa nchini Afrika Kusini amefunguka kuzungumzia ugonjwa unaomsumbua baada wiki iliyoishi kuzagaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba amelazwa katika chumba cha uangalizi wa maalumu ICU.



Muimbaji huyo kupitia Exclusive na Millardayo, amesema kabla ya kwenda nchini Kenya kwa matibabu na baadae Afrika Kusini, alifanyiwa vipimo nchini Tanzania na hospitali na kupewa majibu kwamba atakuwa na kansa ya koo.

“Baada ya kupata shida kwenye kumeza chakula pamoja na maji nikajaribu kufanya vipimo mbalimbali vikiwemo ‘endescope’ ikaonekana kwamba sehemu yangu ya mfumo wa kupitishia chakula umebana, chakula hakishuki. Kwahiyo wakajaribu kupatanua kidogo ili chakule kipite lakini kadri siku zilivyoenda tatizo likazidi kukuwa, nakumbuka nikaenda hospitali moja kubwa Tanzania lakini nilivyokwenda wakanifanyia vipimo wakanimbia bwana wewe, hii ni kansa ya koo, ile siku naambiwa wakati naambiwa nilijikuta kama kilo tano zikapungua ghafla,” alisema Ommy Dimpoz.

Ommy amesema baada ya kwenda nchini Kenya na Afrika Kusni na kufanyiwa vipimo aliambiwa sio kansa bali naonekana alikunywa sumu na hiyo sumu ndio imeweza kuuwathiri mfumo wake wa chakula.

“Tulivyofika Afrika Kusini wakafanya vipimo na wao wakasema sio kansa, nikasema ni nini? wakaniuliza swali ambalo waliniuliza madaktari wa Mombasa, yule daktari akaniuliza haujawahi kunywa sumu? swali ambalo niliulizwa Kenya, niwaambia hapana na hilo swali nimeulizwa na madaktari wangu Mombasa, akanimbia kesi kama yako inasababishwa na sumu,” alisema Ommy.

Alisema baada ya kugundua tatizo hilo alifanyiwa upasuaji nchini humo na kuwekewa mfumo mpya wa chakula na kuachana na mfumo wa zamani ambayo ilikuwa unabana kila mara hata ukitanuliwa.

Kwa sasa muimbaji huyo bado yupo nchini Afrika Kusini kwaajili ya matibabu zaidi kwani bado anaonekana afya yake haijakaa vizuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad