VIDEO:Mashabiki Wamshusha Davido Jukwaani Nchini Namibia, Wahuni Wamvua Saa na viatu


Jana usiku msanii wa muziki kutoka Nigeria, Davido amejikuta akishushwa jukwaani na mashabiki wake waliokuwa wamepagawa na show yake jukwaani kunako uwanja wa mpira wa Sam Nujoma.

Davido ambaye alipanda Jukwaani na msanii mwenzie kutoka Nigeria, RunTown alijikuta akivutwa na mashabiki wake huku walinzi wa show hiyo wakijitahidi kumchomoa kutoka kwa mashabiki hao.

Tayari imeripotiwa kuwa wakati anavutwa na mashabiki hao, wahuni walimvua saa na viatu kitu ambacho kilimfanya ashindwe kuendelea na show.

VIDEO:

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad