"Wachungaji Wenzangu Muache Unafiki, Mimi Kuangalia Filamu Mlimani City sio Dhambi" Nabii Daniel


Nabii Daniel Shilla ambaye amejipatia umaarufu mkubwa mtandaoni kwa kugawa pesa kwa waumini wake na watu mbalimbali, amesema sababu kubwa ya yeye kuwa karibu na wasanii wa filamu nchini ni kutaka kuwaweka karibu na Yesu huku akiwaponda wachungaji wengine kuwa waache unafiki.

 Nabii Daniel amefunguka hayo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV, baada ya yeye kuonekana eneo la Mliman City jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa filamu mpya ya Duma inayoitwa nipe changu.

"Ili mimi niwakamate watu wa bongo movie na niwalete kwa Yesu ni lazima nikae nao karibu, siwezi nikaa nao mbali halafu nitegemee kuwavuta. Mimi Duma ni mtu ambaye nimemsaidia sana katika kazi zake za sana", amesema Nabii Daniel.

Pamoja na hayo, Nabii Daniel ameendelea kwa kusema
"kuangalia filamu sio dhambi tena kuna wachungaji hao walokole wengine ni wanafiki wanaangalia nyumbani ila mimi nimeamua kuangalia 'live".

Mbali na hilo, Nabii Daniel amesema lengo kubwa ya yeye kujichanganya kwa watu mbalimbali ni kutaka kutangaza neno la Mungu, kwa kuwa hata Yesu alivyoshuka duniani alitembelea makundi mbalimbali na kujiweka kwa kila mmoja wao na kutangaza neno.

Mtazame hapa chini Nabii Daniel akifunguka zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad