Wakili Anayewatetea Mbowe na Vigogo Tisa wa Chadema Ajitoa kwenye Kesi

Wakili Anayewatetea Mbowe na Vigogo Tisa wa Chadema Ajitoa kwenye Kesi
Wakili Jeremiah Mtobesya anayewatetea viongozi tisa wa Chadema akiwamo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, amejitoa kwenye kesi hiyo.

Wakili huyo alijitoa kuwatetea washtakiwa hao mara baada ya Mahakama ya Hakimu Kisutu kuyatupilia mbali maombi yao ya kutaka kesi hiyo ya jinai namba 112 ya mwaka huu iahirishwe katika Mahakama ya Kisutu ili kusubiri   maombi yao na rufaa yaliyopo Mahakama ya Rufani yasikilizwe na kutolewa maamuzi.

Hata hivyo Hakimu Mashauri aliyatupilia mbali maombi hayo kwa sababu kifungu cha sheria walichotumia cha 225 (1) (2) cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho2002 hakiipi mamlaka hayo.

Viongozi hao tisa wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwamo  kuhamasisha maandamano Februari 16 mwaka huu siku moja ya uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad