Walevi kukiona sikukuu ya Eid


Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo amewaonya madereva kuacha kutumia vilevi huku wakiendesha vyombo vya moto kwa kutumia kigezo cha Sikukuu. 

Murilo ametoa onyo hilo kwenye mahojiano na East Africa Breakfast ya East Africa Radio ambapo amesema kuwa Sikukuu zipo siku zote na zisitumike kama kigezo cha kufanya anasa zinazopelekea madhara kwa jamii, kama vile kutumia vilevi kupitiliza na kuacha watoto kutoka majumbani bila uangalizi. 

“Sikukuu haimaanishi kwamba ndio mtumie pombe halafu muendeshe vyombo vya moto, haimaanishi mtoke majumbani wote ili mtoe mianya kwa wezi kuingia majumbani, au ndio kigezo cha kuwaacha watoto watoke peke yao, hii sio maana ya Sikukuu kwani vitu vingine sio vya lazima”, amesema Kamanda Murilo. 

Kamanda Muliro amesema kuwa hakuna vituo vya Polisi vitakavyofungwa sababu ni Sikukuu bali viko wazi muda wote na atakayevunja sheria atakamatwa na kufikishwa mahakamani siku za kazi kama kawaida. 

Takwimu za Jeshi la Polisi zinaonesha kuwa matukio mengi ya ajali zinazotokea siku za Sikukuu husababishwa na uzembe wa madereva kwa kisingizio kuwa ni siku ya kusherehekea na kunywa pombe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad