Walickosema Humphrey Polepole na Bashe Baada ya Julius Mtatiro Kutoka CUF Na Kujiunga CCM

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro amejivua uanachama wa chama hicho nakujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM leo Agosti 11, 2018.

Mtatiro ametaja mambo matano yaliyomfanya atoke CUF na kujiunga CCM  ambayo ni pamoja na, mosi kutoridhishwa na hali ya ushiriki na mchango wake kwenye siasa za CUF, pili ni mgogoro wa kiuongozi unaoendelea kukikumba chama hicho.

Jambo la tatu ni kutoridhidhwa na ushiriki wake kama kijana na kiongozi katika kuchochea maendeleo ya nchi. Wakati jambo la nne likiwa ni ajenda ya maendeleo ya nchi, huku jambo la mwisho likiwa ni mustakabali wake kuhusu masuala ya siasa.

Makada, Wabunge  wa CCM na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini wametoa maoni tofauti kuhusu uamuzi wa Mtatiro  kuhama CUF na kwenda CCM.

Mbunge wa Kigoma Mjini, (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe ameandika kwenye ukurasa wake wa Twita akisema:

“Huko wanakokutegea kukufukuza kila usemapo ukweli? Ninaamini kwenye maendeleo ndani ya Demokrasia na siyo maendeleo ndani ya udikteta. Ninaamini katika uhuru wa fikra na siyo mawazo ya kiimla.Ninaamini nchi yetu inahitaaji chama kingine kuirudisha kwenye reli. Nafasi ya CCM ni Museum (makumbusho)."

Ndipo Mbunge wa Nzega, (CCM) Hussein Bashe akaamua kumjibu Zitto Kabwe kwa kuandika;  “Ni rahisi kuleta mabadiliko ya haki, demokrasia na maendeleo ndani ya CCM) kuliko kutafuta mabadiliko nje kwa sababu kuna mgogoro wa kimawazo, kimuundo na kimadili huko nje. Kuna wanajeshi wachache wa ukweli.”

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole yeye kafunguka na kusema hata yeye kayakuta mtandaoni. ameandika;“Huu unaitwa uhuru wa kisiasa kwa mujibu wa katiba yetu, halafu wale wa ‘siasa za bei nafuu mseme kanunuliwa;” Hongera kaka, ndugu, kamaradi. Historia na Mungu pekee atakupa tuzo ya dhamira yako njema. Na mimi nimeikuta mtandaoni.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad