Kikosi kimoja cha majeshi ya Nigeria kimefyatua risasi angani kupinga amri ya kwenda mstari wa mbele kukabiliana na wanamgombo wa Boko Haramu.
Vyombo vya habari vya nchi hivyo vimeripoti kuwa askari alikataa kupanda ndege ambayo ilikuwa iwahamishe kutoka Maiduguri katika mji mkuu wa jimbo la Borno kwenda katika mji wa Marte karibu na nchi jirani ya Niger.
Hali hiyo hakutarajiwa lakini ndivyo ilivyotokea katika jeshi la Nigeria siku ya jumapili, ambapo wanajeshi wa kikosi kimoja walipoonyesha kukataa kwenda mstari wa mbele kukabiliana na Boko haramu.
Mwandishi wa BBC anasema kumekuwepo na hali ya kutotii amri miongoni mwa wanajeshi kwa miaka nane sasa.
Kundi la Boko haramu limekuwa liikiendesha vitendo vya utekaji mauaji na hata vitendo vya ubakaji na ukatili.
Kumekuwa na maswali mengi kutoka miongoni mwa raia kufuatia kundi hilo kuendelea na vitendo vya kikatili huku majeshi Nigeria yakidai yanalidhibiti.