Wanakijiji 68 Watiwa Mbaroni kwa Kuharibu Miundo Mbinu, Ni Wale Ambao RC Mbeya Aliagiza Wakamatwe



Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 68 kati yao 62 ni wanaume na 06 ni wanawake kwa tuhuma za kufanya uharibifu wa miundombinu ya maji huko katika Kijiji cha Ngole kilichopo Kata ya Ilungu, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Katika msako mkali uliofanywa mnamo tarehe 17.08.2018 kuanzia majira ya saa 10:00 asubuhi hadi saa 18:00 jioni huko katika Kijiji cha Ngole jumla ya watuhumiwa 68 walikamatwa.

Awali mnamo tarehe 14.08.2018 kuanzia majira ya saa 10:00 asubuhi huko katika Kijiji cha Ngole, Kata ya Ilungu, Tarafa ya Tembela watuhumiwa hao kwa makusudi na bila halali waliharibu mabomba na vyanzo vya maji kwa kutumia silaha za jadi na kusababisha hasara ya takribani Shilingi Milioni 14 mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni michango ya baadhi ya wanakijiji na wafadhili.

Watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwanadamizi wa Polisi ULRICH MATEI anatoa msisitizo kwa watanzania na wana Mbeya wote kuhakikisha wanalinda rasilimali zetu zikiwemo miundombinu ya afya, elimu, barabara, maji na nishati ili kufikia malengo tarajiwa ya uchumi wa viwanda.

Pia Kamanda MATEI anatoa rai yeyote atakayeharibu miundombinu hiyo Polisi tutamkamata na kumfungulia shitaka la kuhujumu uchumi [Sabotage] na kuhakikisha wanafikishwa Mahakamani.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na Operesheni mbalimbali, doria katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha hali ya Mkoa inakuwa shwari ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa magari, kuwapima kilevi madereva pamoja na kuendelea kutoa elimu ya matumizi salama ya barabara kwa makundi mbalimbali ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

               Imetolewa na:             
 [ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad