Wanasiasa Wanaong'ang'ania Kukaa Kwenye Chama Kimoja kwa Muda Mrefu Bila Kuhama ni ‘Manungayembe’ – Mwita Waitara

Wanasiasa Wanaong'ang'ania Kukaa Kwenye Chama Kimoja kwa Muda Mrefu Bila Kuhama ni ‘Manungayembe’ – Mwita Waitara
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Ukonga kwa tiketi ya CHADEMA, Mwita Waitara amedai kuwa wanasiasa wanaong’ang’ania kukaa kwenye chama kimoja kwa muda mrefu hao ni Manungayembe’.


Mwita Waitara kushoto kwenye picha.
Waitara amesema kuwa ukiona mwanasiasa kwa miaka yote haoni mafanikio wala maendeleo kwa kupinga kila kiongozi anayeingia madarakani basi ujue huyo ni Nungayembe.

Akifafanua kauli hiyo kwenye kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Mwita amesema kuwa kuna viongozi kuanzia awamu ya Mwinyi walikuwa wanaipinga serikali, awamu ya Mkapa hivyo hivyo, awamu ya Kikwete wanapinga na ya Rais Magufuli wanapinga tu ujue hao ni Manungayembe kwani mwanasiasa wa kweli ni lazima abadilike kuendana na mazingira.

Hata hivyo, kauli hiyo haijaeleweka kuwa amemulenga nani. Mwita alijiengua CHADEMA na kutangaza kujiunga Chama tawala cha CCM kwa kudai kuwa anaunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Mwita pia ameteuliwa na Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa ya CCM kugombea Ubunge kwenye jimbo hilo la Ukonga na ameahidi kuchukua jimbo hilo kwa kishindo akidai kuwa anakubalika na wananchi wa jimbo hilo wameanza kukielewa Chama cha Mapinduzi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad