Watanzania Acheni Kupotoshwa, Mtanzania Anayejua Kiingereza Ameelimika Kuliko Asiyejua

Kuelimika maana yake ni kuwa na maarifa ama kujua vitu vingi vyenye kukusaidia kuyajua mazingira na kukabiliana na changamoto zake kuliko awali

Mtanzania anayejua Kiingereza inaamisha anajua lugha moja zaidi kuliko asiyejua [anajua Kiswahili na Kiingreza] maana kiswahili ndio lugha yake ya nyumbani, na Kiingereza amabayo ni lugha nyingine ya ziada itakayomsaidia kuijua mazingira na dunia zaidi

Huyu asiyejua Kiingereza {anajua Kiswahili na lugha mama tu}, inamaanisha hana skill za kuelewa mambo mengi kwa sasa ambayo yapo katika lugha ya Kiingereza na hivyo amezidiwa elimu.

hata kwenye kuajiri ,muajiri hata kama anamuajiri shamba boy au housegirl, au anaajiri Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni, atampa nafasi mwenye kujua Kiingereza kuliko asiyejua, shamba boy anayejua Kiingereza ataweza kusoma hata maelezo ya kwenye dawa ama chakula cha mifugo na kufanya kazi kwa utaalamu unaotakiwa zaidi, housegirl anaweza kusoma hata njia salama ya kutumia vifaa vya umeme n.k



Mjadala uliooendeshwa na HakiElimu

Siku za karibuni, HakiElimu waliendesha mjadala kuhusu lugha inayotakiwa kufundishia kwenye shuleni hadi vyuo vikuu, mjadala huu haukufikia tamati, pia nimesikia mjadala huu ukiendeshwa kwenye kituo fulani cha redio leo asubuhi

Wachangiaji wengi wanaounga mkono Kiswahili kitumike hadi elimu ya juu point zao ni kuwa Kiingereza sio utamaduni wetu, wengine wanasema pia Kiswahili kitakua kirahisi kufundishia

Kiingereza Sio Utamaduni Wetu

Wanaoshikilia Kiingereza sio utamaduni wetu na ni mfumo wa ukoloni mamboleo hivyo hakifai kutumika, hawajajiuliza mbona tuna dini ambazo sio utamaduni wetu? mbona mfumo wa utawala sio utamaduni wetu? mbona kuna mifumo mingi sana kuanzia afya, elimu kiujumla, mavazi hadi nyumba zetu ambazo sio utamaduni? hii mifumo tuiache kwa sababu ni ukoloni mamboleo? na kwani utamaduni ni kitu gani anyway? utamaduni ndio unaboresha maisha ya watu?

Utamaduni ndio utakuwezesha kuwa na viwanda vyako mwenyewe? ndio utakusaidia kuboresha kilimo, afya, na makazi bora?

Na wachangiaji waliokuwa wakisema Kiingereza sio utamaduni wetu hao hao wamewapeleka watoto wao shule za Kiingereza na wakiongea utawasikia wakichanganya Kiingereza na Kiswahili [Swanglish] kwenye mazungumzo yao hadi wanakera. Unafiki ulioje


Ukijifanya unangang'ania utamaduni wako unaweza kujikuta unarudi kwenye zama za mawe huku wenzako wanaojichanganya na dunia wakisonga mbele


Kiingereza Kinachangia Wanafunzi Kufeli

Kingine ni kuwa kuwafundisha kwa Kiingreza wanafunzi wetu sekondari ambao msingi wao ulikuwa ni Kiswahili ndio kinachowafanya wasifaulu..

Hili nalo sijui lina ukweli gani kwani mwanafunzi kama anazingatia masomo na kujifunza kweli lugha itamsumbua tu akiwa kidato cha kwanza, maana lugha sio kitu kigumu sana kujifunza hata.

Hata wale wanaoanza kidato cha kwanza wakiwa na advantage ya kujua Kiingereza huwa sio wanaoongoza darasa hadi, wanaweza kuongoza form one pale mwanzo ila wanakuja kupitwa tu

Na kama Ingekuwa Lugha ndio tatizo sana mbona ufaulu wa somo la Kiswahili hautofautiani na masomo mengine? mwaka tuliomaliza shule somo la Civics ndio lililoongoza kwa watu kufaulu na sio Kiswahili

Hata ukicheki kitaifa Kiswahili halijatofautiana na masomo Mengine kwa ufaulu

Hata kama lugha ingekuwa ni tatizo kwani tusingeweza kuanza kuwafundisha kwa kiingereza kuanzia shule za awali? maana wanaosoma shule za msingi kwa Kiingereza wakifika sekondari hawaangaishwi na lugha lakini hata hawaongozi darasa pia!

Na hata kama hili ni tatizo basi tungeanza taratibu kuifanya kiingereza kuwa lugha ya kufundishia shule za msingi, tukianza sasa hivi ndani ya miaka 15 hivi tutakuwa tumeshaweza kufanya hili

Na haimaanishi kuwa tutakuwa tunaitupa ;lugha yetu ya kiswahili, hii ni lugha amabayo tuanitumia nyumbani kila siku na bado itakuwa inafundishwa shuleni kuanzia msingi hadi sekondari
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad