Watetezi Haki Za Binadamu Walaani Mnyeti Kumtupa Selo Wakili

Watetezi Haki Za Binadamu Walaani Mnyeti Kumtupa Selo Wakili
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umelaani kitendo cha kushikiliwa kwa Wakili Menrad D’Souza na wateja wake kwa amri ya Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti juzi Julai 30, mwaka huu.

Mratibu wa Mtandao huo, Onesmo Olengurumwa amesema kitendo hicho ni ukandamizaji wa haki na uvunjwaji wa katiba ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Agosti Mosi, Jijini Dar es Salaam Olengurumwa amesema kuwa hawakufurahishwa na kitendo hicho hivyo wanalaani kwa nguvu zote na kuwataka wakuu wa mikoa na wilaya kufanya kazi kwa mujibu wa katiba.

“Wakili huyo alifungiwa katika chumba kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa Manyara juzi, kutokana na madai ya kushinikiza wakili na wateja wake waweze kuwasiliana na wakurugenzi wa wateja hao ili wakubali kuongeza kiasi cha fidia kwa wakulima katika mgogoro wa mbegu kati yao na wateja wa wakili D’Souza.

“THRDC kama mwavuli wa watetezi wa haki za binadamu inatambua kuwa mawakili ni watetezi wa haki za binadamu na wanafanya kazi zao za utetezi kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na nchi,” amesema.

Kutokana na hilo, ameshauri kwamba ikitokea kuna wakili viongozi anadhani amekiuka maadili ya kazi yake basi atoe taarifa kwa chama cha mawakili au mahakama.

Pia kwa mawakili amewasihi  kupitia vyama vyao wasimame kwa umoja na kulinda Uhuru wa kazi ya mawakili na utawala wa sheria hapa nchini.

Sambamba na hilo, Mratibu huyo amewaomba wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuacha kutumia madaraka yao chini ya kifungu cha 15 na 17 cha sheria ya Tawala za Mkkoa ya mwaka 1996 kwa kutoa amri ya kuwakamata watu na kuwaweka vizuizini bila sababu za msingi za kisheria kwani vitendo hivyo vimekuwa vokijirudia mara kwa mara.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad