Polisi nchini Uganda inasema imewakamata watu 103 katika maandamano yaliozuka kupinga kukamatwa kwa mbunge wa upinzani Robert Kyagulanyi au Bobi Wine pamoja na wabunge wengine kadhaana wanaharakati nchini Uganda.
Vikosi vya usalama nchini Uganda vilizima maandamano kwenye mji mkuu hapo jana Kampala kupinga kukamatwa kwa Bobi Wine .
Waandamanaji wamechoma moto magurudumu ya magari, wanarusha mawe huku pia wakiweka vizuizi vya barabarani.
Bobi Wine alikamatwa na kushtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi wiki iliyopita
Wanajeshi na polisi walionekana wakiwa juu ya magari wakipita kati kati mwa mji. Sehemu nyingine za mji wa kampala maafisa wa usalama wamefyatua risasi hewania na kurusha vituo machozi kutawanya waandamanaji.
Misukosuko inaongezeka mjini Kampala kufuatia kukamatwa kwa mbunge Bobi Wine. Ripoti zimeibuka kuwa aliteswa akiwa mikononi mwa wanajeshi. Rais Yoweri Museveni amekana madai kuwa Bobi Wine alijeruhiwa.
Wiki iliyopita Bobi Wine 32, na watu wengine walishtakiwa baada ya kampeni za kuelekea uchaguzi mdogo eneo la Arua kaskazini mwa nchi. Polisi wanasema walikuwa wamewaongoza wafuasi wao kushambulia msafara wa Rais Museveni.