Rapper Young D amezungumza ishu ya yeye kufunga ndoa ikiwa ni baada ya kutoa wimbo wake mpya wa ‘Naoa’ ambapo Young D amesema kwamba anashangaa kuona watu hawajaamini yeye alivyosema anaoa lakini wakati alivyotoa wimbo wa ‘Dada anaolewa’ watu waliamini.
Hata hivyo Young D amesema kitendo cha watu kumjadili kuwa yeye hawezi kuoa imemfanya ajishangae na kuendelea kujitathimini na kumuongezea utamani wa kufunga ndoa sababu wapo watu waliosikia anafunga ndoa waka muheshimu.
YOUNG D…>>>“Najiuliza kwani bado na maseke mengi au..? au watu hawapendi nioe..? Najaribu kujitathimini ila watu wajue kwamba dalili ya mvua ni mawingu..”
Watu Hawapendi Nioe, Najaribu Kujitathimini- Young D
0
August 29, 2018
Tags