Zaidi ya watu 21,000 wamehamishwa kutoka kwa njia ya moto unaokaribia kwa kasi Kusini mwa California.
Kuhama huku kwa lazima kulifuatia amri kutokana na kwamba moto huo kwa jina Moto Mtakatifu, ulitishia nyumba kadhaa kando mwa ziwa Elsinore kaunti ya Orange.
Moto huo ambao ni moja ya mingi kote jimboni humo umeharibu zaidi ya ekari 19,000 za msitu Kaskazini mwa San Diego.
Mwanamume mmoja anayeshukiwa kuanzisha moto huo mtakatifu amefikishwa mahakamani.
Forrest Clark alifoka mara kadhaa alipofikishwa kwenye mahakama ya Kaunti ya Orange mara nyingine akificha uso wake.
Kesi yake ilihairishw hadi tarehe 17 Julai Agosti na dhamana imewekwa dola milioni moja.
Mamlaka zinasema kuwa alianzisha moto huo makusudi siku ya Jumatatu bada ya muongo mmoja wa mvutano na majirani.
Kulingana na maafisa wa Kaunti ya Orange, Bw Clark alikuwa amemtumia barua pepe mzima mtoto wa kujitolea akitisha, "eneo hili litachomeka
Zaidi ya wazima moto 6000 wanapambana na moto huo ukiwa ni kati ya mioto 18 iliyo kwa sasa jimbo la California.
Moto unaofahamika kaam Mendocino Complex umetangazwa kuwa mkubwa zaidi kweny historia ya jimbo hilo na tarayi umechoma akari 290,692.
Maafisa wa moto wanaaminiwa moto huo kuendelea kuwaka kwa mwezi mzima.
Moto mwingine - tha Carr Fire ulio kaskazini, umewaua watu saba na kuharibu zaidi ya nyumba 1,500.
Kote jimboni humo takriban wazima moto 14,000 wanajikakamua kupambana na visa vingie vya kuzuka kwa moto.