Waziri Jafo Awaonya Ma-DC Wanaotumia ‘Kiki’ ya Kuwaweka Watu Ndani Masaa 24

Waziri Jafo Awaonya Ma-DC Wanaotumia ‘Kiki’ ya Kuwaweka Watu Ndani Masaa 24
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi) Selemani Jafo amewataka wakurugenzi wapya kuepuka kujiingiza katika ugomvi wa kisiasa utakaokuwa chanzo cha kushindwa kutekeleza majukumu yao huku pia akituma ujumbe wa wakuu wa wilaya ambao wanapenda kiki za kuwaweka ndani baadhi ya watu.


Amesema hayo leo Agosti 14, 2018 wakati wa hafla ya kuwaapisha wakurugenzi wapya mjini Dodoma.

Jafo amesema kiki za ajabu za kuwakamata na kuwatia watu ndani bila sababu hupelekea watu kuichukia Serikali yao.

“Lakini kumetokea na tendency, Mkuu wa wilaya anaona kiki kubwa sana ni kuwatiwa watu ndani masaa 48. Hiyo ni kiki kumbe kulikuwa na kiki nyingi ukiwa kama mkuu wa wilaya,” alisema Jafo.

“Kuwatia ndani watu inawezekana inasababishia hata serikali kuchukiwa na serikali kwa sababu ya kuwatia watu ndani bila kuwa na sababu za msingi,” aliongeza Jafo.

Naye katibu mkuu Tamisemi, Mussa Iyombe amewataka wakurugenzi wapya kuhakikisha kuwa wanatenga muda wa kuzungumza na watumishi badala ya kuwaachia maofisa utumishi ambao wamekuwa wajeuri

“Mkurugenzi haingii ofisini, anatafutwa na waziri hapatikani, katibu mkuu hapatikani inashangaza. Wanawaachia maofisa utumishi wawasikilize watumishi, wajeuri kweli kweli wanaharibu sifa zenu. Kumuona mkurugenzi afadhali uende mbinguni na ukienda utakuwa umekufa,” amesema
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad