Waziri Lugola Awakalia Kooni Polisi " Nikikukuta Umembambikia Mtu Kesi, Umechukua Rushwa Nakuweka Ndani"

Waziri Lugola Awawashia Taa Nyekundu Polisi " Nikikukuta Umembambikia Mtu Kesi, Umechukua Rushwa Nakuweka Ndani"
Siku chache baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kumweka mahabusu Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara mjini, Ibrahim Mhando, leo Jumanne Agosti 28, 2018 amesema ataendelea na utaratibu huo kwa askari wanaotesa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kangi amewaonya askari polisi wanaowabambikia kesi wananchi akisema hawajui siku wala saa atakayowafikia.

"Nimeanza kutembelea vituo vya polisi, nimesema hakuna kituo cha Polisi ambacho sitafika. Ili nijionee utendaji wa polisi, wananchi na wananchi wanavyohudumiwa," amesema.

"Ili kuona wananchi wanaodaiwa kubambikiwa kesi na watu wasio waaminifu. Popote nitakapokuta hao askari wanaotuchafulia nitawachukulia hatua za papo kwa papo."

Amesema, “nimekukuta wewe askari umembambikia kesi, umechukua rushwa, basi nakuingiza na wewe hapo uone hasara ya kulichafua jeshi."

Amesema ameshamwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro kuwachukulia hatua askari hao ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi.

"Mimi ni mkristo na ninasoma biblia, inasema hakuna anayejua siku wala saa atakayokuja mwana wa adamu yaani maana wa Mungu," amesema.

"Askari msifikiri vituo hivi ni vingi, hamjui siku wala saa atakayokuja Ninja," aliongeza Kangi.

Pia, amewaonya askari wa usalama barabarani akisema wamekuwa wakikamata magari ya abiria yakiwa na abiria kwa makosa ya dereva na kuyapeleka vituoni.

"Matokeo yake wanawachelewesha abiria, wengine wanaenda kwenye kesi zao, wengine wanatafuta kazi, wengine matibabu, wengine kwenye misiba," amesema.

“Nimemwelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi kwamba wamiliki wa magari wanafahamika. Tusitumie kisingizio cha kukusanya fedha kukamata magari yakiwa na abiria."

Amewataka askari hao kukamata madereva peke yao wasiwasumbue wananchi wasio na hatia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad