Waziri Mkuu wa Australia Malcom Turnbull Atimuliwa

Waziri Mkuu wa Australia Malcom Turnbull Atimuliwa
Scott Morrison anatarajiwa kuwa waziri mkuu mpya wa Australia baada ya Malcom Turnbull kutimuliwa kwa lazima na chama chake maafisa wamethibitisha.

Turnbull alikuwa kwenye shinikizo kubwa kuanzia kuorodheswha chini katika kura za kutafuta maoni, uchaguzi unaowadia, na kugeukiwa na wabunge wa kihafidhina.

Morrison ambaye ndiye mweka hazina wa sasa alishinda kura 45 kati ya 50 ya ndani dhidi ya waziri wa mambo ya ndani Peter Dutton amaesema kinara wa chama cha kiliberali Nola Maroni.

Turnbull hakuwania katika ushindani huo wa uongozi.

Alikubali kuandaa kura baada ya idadi kubwa ya wabunge katika chama chake kusaini barua kutaka uchaguzi ufanyike.

Turnbull alikuwa akipuuzia wito wa kumtaka ajiuzulu wakati tuhuma za uongozi zikiididimiza serikali yake.


Jana Alhamisi , aliwaambia waandishi habari, kuwa raia nchini Australia 'watashangazwa mno kwa wanachokishuhudia'.

Waziri wa mambo ya nje Julie Bishop pia ni miongoni mwa waliogombea nafasi hiyo, lakini hakufanikiwa katika duru ya mwisho.

Bwana Turnbull na Bi Bishop hawakuzungumza na waandishi habari moja kwa moja baada ya kura hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad