Waziri Mkuu wa Uingereza Atua Kenya Katika Kuboresha Biashara na Afrika

Waziri Mkuu wa Uingereza Atua Kenya Katika Kuboresha Biashara na Afrika
Uingereza ina uhusiano wa kihistoria na mataifa mengi ya Afrika. Uhusiano huo bado unaendelea kuwa na maana, lakini kitu kimoja ambacho Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amekutana nacho katika ziara yake ya Afrika ni kuwa nchi yake inagombea nafasi na mataifa mengine yanayowekeza kwa kiwango kikubwa.

Hii leo Bi May ametua Kenya baada ya kuzuru Afrika Kusini na Nigeria. Hii ni ziara ya mwanzo kwa Bi May barani Afrika akiwa mamlakani. Nchi yake imenuwia kuimarisha mahusiano yake na mataifa ya Afrika kipindi hiki ambacho wanakaribia kujitenga na Umoja wa Ulaya (EU).

Akiwa jijini Cape Town, Bi May ameahidi nchi yake kuwekeza pauni bilioni 4 barani Afrika mara baada ya nchi yake kuondoka EU mwakani.

May pia amesema anatarajia kusain makubaliano na serikali ya Kenya kurejesha mabilioni ya pesa yaliyotoroshewa Uingereza kinyume cha sheria.

"Azma ya Uingereza baada ya kujitoa EU mwezi Machi 2019 ni kuimarisha ushirikiano wake na dunia kwa ujumla…Wiki hii natarajia kuwa na mjadala wa namna gani wa kufikia azma hiyo pamoja na bara la Afrika kwa kusaidia katika uwekezaji wenye tija na kukuza ajira pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama," ilisema sehemu ya taarifa ya Bi May kabla ya ziara yake.

Kabla ya May kuwasili Kenya, rais wa taifa hilo Uhuru Kenyatta alikuwa Marekani ambapo alifanya mazungumzo na rais Donald Trump na wawili hao kusaini makubaliano kadha ya kibiashara yenye thamani ya $900 miloni.

Baada ya kukutana na Bi May, Bw Kenyatta ataelekea Uchina kwenda kushiriki mkutano wa uhusiano baina ya Uchina na Afrika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad