Yanga sio wa Kimataifa Tena...Washika Mkia Kombe la Shirikisho


BAADA ya kumalizika kwa michezo ya kundi D, ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika hatimaye klabu za Yanga na Gor Mahia zimeaga rasmi michuano hiyo baada ya kupoteza katika michezo yao ya mwisho. Anaripoti Kelvin Mwaipungu …. (endelea).

Yanga ilipoteza mchezo wake mbele ya Rayol Sport ya Rwanda kwa kukubali kipigo cha bao moja kwa bila lililofungwa dakika 19, ya mchezo na mshambuliaji Bimenyimana baada kutumia vizuri makosa yaliyofanywa na Nahodha wa klabu hiyo Kelvin Yondani.

Kwa upande wa Gor Mahia ambayo ilikuwa ugenini mbele ya USM Alger ilikubali kipigo cha mabao mawili kwa moja, mabao ya mchezo huo kwa upande wa wenyeji yalifungwa na Price Ibara dakika ya 36 na Sayoud aliyefunga dakika ya 81 ya mchezo huku bao pekee la wakenya hao lilifungwa na Tuyisenge 83.

Kwa matokeo hayo, USM Alger ikiwa na pointi 11 kileleni, na Rayon Sports yenye pointi 9, zinafuzu hatua ya robo fainali, huku Gor Mahia ikipata alama 8, na kushika nafasi ya tatu na Klabu ya Yanga iliambulia alama nne na kushika mkia kwenye kundi hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad