Muigizaji wa filamu bongo, Yusuph Mlela amefunguka na kudai uwepo wa 'bifu' baina ya Gabo na Duma umewapa faida kubwa kwenye tasnia yao, kwa kuwa bongo movie ilikuwa imepwaya lakini kwa sasa imeanza kuchangamka kutokana na hilo.
Mlela amebainisha hayo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE 'FNL' kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, na kusema kwamba ugomvi ni njia pekee inayoweza kuchangamsha soko la filamu kwa kuwa unakuwepo ushindani wa kazi kwa namna moja ama nyingine.
"Sio kitu kibaya kuwepo na bifu, unajua 'game' letu lilikuwa limepoa kwa kiasi fulani, hivyo uwepo wa ugomvi wao inachangamsha tasnia pamoja na kukuza. Tunapenda kuona hivyo angalau bongo movie inakuwa inazungumziwa", amesema Mlela.
Pamoja na hayo, Mlela ameendelea kwa kusema kuwa "nawashauri wasiifanye kiubaya ila waifanye kwa faida ili iwaletee mafanikio na iwe kama mbele wenzetu wanavyofanyaga".
Ugomvi baina ya Gabo Zigamba na Duma ambao wote ni wasanii wa bongo movie ulianza tokea mwaka 2016, mara baada ya Gabo kushinda tuzo ya 'EATV AWARDS' katika kipengele cha muigizaji bora wa kiume ambao waliokuwa wakishindanishwa zaidi ya wasanii wanne akiwepo na Duma katika watu hao, na kupelekea kuanza kutoa maneno yenye kashfa katika siku za mbele yake kuwa hautendei haki ustaa wake kwa madai hajui kuvaa wala kuishi kistaa.
Yusufu Mlela Afulahia Uwep[o wa Bifu la Duma na Gabo
0
August 25, 2018
Tags