Zoezi la uhakiki wa leseni za madereva lasitishwa

Zoezi la uhakiki wa leseni za madereva lasitishwa
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Fortunatus Muslim amesitisha zoezi la uhakiki wa leseni lililoanza hivi karibuni hadi utakapotangazwa tena huku akitoa muda kwa madereva kwenda kusoma.


Kwa mujibu wa Azam TV, Muslim wiki hii ametoa tamko hilo jijini Dar es Salaam wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua utendaji kazi wa watendaji walio chini yake.

Kuhusu wanaokamatwa na makosa ya barabarani, Kamanda Muslim amesema gari yoyote itakayokamatwa kama ina madeni basi dereva wake asiandikiwe faini bali akamatwe na kufikishwa mahakamani.


“Dereva au gari itakayokamatwa kwa makosa ya usalama barabarani na kama anamadeni, asiandikiwe, apelekwe moja kwa moja mahakamani,” alisema kamanda Muslim wakati akitoa somo kwa madereva na wamiliki wa magari.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad