Abiria 35 waliokuwa wakisafiri katika ndege ya Shirika la Niugini na wafanyakazi 12 wamenusurika kifo baada ya ndege hiyo kuanguka baharini baada ya kushindwa kutua katika uwanja wa kimataifa wa Weno, Micronesia.
Ndege hiyo aina ya Boeing 737 ilikuwa inataka kutua kwenye uwanja hao lakini ilipitiliza uwanja na kutumbukia kwenye wangwa wa kisiwa cha Chuuk Ijumaa asubuhi.
Kabla ya ndege hiyo kuzama nusu abiria na wafanyakazi hao walilazimika kuogelea kuokoa maisha yao katika kisiwa hicho kilichoko katika bahari ya Pacific.
Msemaji wa shirika hilo, ambalo ndege yake ilikuwa katika safari za kawaida na ikijaribu kutua ikitokea Pohnpei mji mkuu wa Micronesian ikielekea Port Moresby, lakini "ilishindwa kutua kwenye uwanja wa kukimbilia".
"Shirika la ndege la Niugini linaweza kuthibitisha sasa kwamba watu wote waliokuwemo ndani waliokolewa salama,” ilisema taarifa fupi ya shirika hilo.