Afanyiwa Operation ya Tumbo na Kukutwa na Kijiko, Mswaki, Kalamu na Vingine


Hospitali teule ya Mugana iliyoko Wilayani Missenyi imefanikiwa kumfanyia upasuaji kijana mmoja mgonjwa akili mkazi wa Kyerwa mkoani Kagera nakumkuta na vifaa mbalimbali tumboni ikiwemo mswaki, kijiko, betri ndogo, kalamu, viberiti vya gesi, mfuko, vitambaa pamoja na mkono wa mashine ya kunyolea ndevu

Mganga Mkuu Wa Wilaya Missenyi Dr Khamis Abdallah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakumtaja mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji nakukutwa vitu hivyo tumboni kwake kuwa ni Robert Novato mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Kyerwa Mkoani Kagera nakwamba ni mgonjwa wa akili kwasasa anaendelea na matibabu katika hospital ya Mugana

Baadhi ya wananchi Wilayani Missenyi wanajiuliza ni kwa jinsi gani vitu hivyo viliingia tumboni,licha ya historia ya kijana huyo kujulikana kwamba ni mgonjwa wa akili Wengine wakiamini kuwa alimeza vitu hivyo mwenyewe Wengine wakiamini katika ushirikina .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad