Msanii na mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva, Akili The Brain amesema ukimya wake katika muziki ulitokana na yeye kuwaacha wasanii wenzake watangulie kutoa kazi zao pamoja na kusoma soko jinsi lilivyo kusudi aweze kuachia ngoma zake.
Akili The Brain amebainisha hayo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha PLANET BONGO 'PB', inayorushwa na East Africa Radio, muda mchache alipomaliza kutambulisha wimbo wake mpya wa 'mashallah'.
"Kabla sijaachia ngoma yangu, nilifanya 'research' kidogo juu ya watu wanataka kitu gani kwa sasa, pamoja na namna muziki jinsi ulivyo kwa sasa. Naweza kubadilika kutokana na 'time' inavyokwenda kusudi niweze kuwapa kile wanachokihitaji watu", amesema Akili.
Pamoja na hayo, Akili ameendelea kwa kusema kuwa "nina 'plan' kubwa ninayotaka kuifanya lakini kwa sasa siwezi kuiweka wazi, kwasababu kuna baadhi ya mambo bado hayajakaa sawa ila Mungu akijalia kila kitu kitakuwa sawa tu".
Mbali na hilo, Akili The Brain ameweka wazi kuwa mara nyingi hupendelea kuwatumia waandishi kuandika mashairi ya ngoma zake, kwa lengo la kutaka kuwatendea haki mashabiki zake.
Akili The Brain ni miongoni mwa wasanii walioweza kuiteka jamii katika miaka ya 2006 kwa vibao vyake kama Bongo Bhangra, Nakupenda Regina na nyingine nyingi.
Akili the Brain Afunguka Kilichompoteza kwenye Game
0
September 05, 2018
Tags