Alichokisema Steve Nyerere Baada ya Wasanii Kupigwa Chini na CCM "Tulifanya Kazi Kubwa Sana Rais Alitupongeza"

Alichokisema Steve Nyerere Baada ya Wasanii Kupigwa Chini na CCM "Tulifanya Kazi Kubwa Sana Rais Alitupongeza"
Siku chache baada ya chama cha mapinduzi CCM kutangaza kuwa hakitawahitaji kuwatumia wasanii katika shughuli zozote za chama Msanii wa filamu za bongo Steve Nyerere ameonyesha kuumizwa na hatua hiyo na kusema kuwa wasanii walifanya kazi kubwa.

Kauli hiyo aliitoa katika ukurasa wake wa instagramu ambapo Steve alituma Picha nyingi na zilizowaonyesha wasanii mbalimbali wakiwa wamevalia mavazi ya chama cha mapinduzi na kuandika maneno yaliyojirudia katika kila post aliyoituma huku yakisomeka 'Walifanya KAZI KUBWA SANA'.  


Steve akuishia hapo aliendelea kuweka picha nyingine akiwa na mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli na Kuandika "Tulifanya KAZI KUBWA SANA, mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wetu alitupongeza''.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad