Alikiba Afunguka Kinachomkwamisha Kuanza Kucheza


Nyota wa muziki nchini ambaye hivi sasa amegeukia kwenye soka Alikiba, amesema yeye binafsi ndio amemuomba kocha wa Coastal Union asicheze ili ajiimarishe zaidi.


Alikiba ameyasema hayo leo baada ya kushindwa kuonekana kwenye mchezo wa 7 wa timu yake ambayo imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbao FC kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Mkwakwani jijini Tanga.

''Nafanya mazoezi sana kabla ya kucheza ili nikianza kucheza watu wajue kweli Alikiba ni mchezaji na sio kwamba nimekuja kujifurahisha, nimemwomba kocha wangu Juma Mgunda na amenielewa'', amesema Alikiba.

Alikiba ameeleza kuwa kitu kingine kikubwa kilichomfanya asionekane kwenye mechi saba za kwanza za ligi kuu msimu huu, ambazo Costal imecheza ni kutaka kuzoeana na wenzake ili kutengeneza muunganiko uwanjani.

Mdhamini huyo wa Coastal kupitia kinywaji chake cha Mo fire, ameweka wazi kuwa kwasasa tayari ameshaanza kuendana na wenzake na muda si mrefu atacheza mechi yake ya kwanza.

Coastal ambayo imerejea ligi kuu msimu huu baada ya kushuka mwaka 2016, mpaka sasa ina alama 10, ikiwa katika nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi ambayo ina jumla ya timu 20.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad