Alikiba, Samatta Watajwa Kwenye Orodha ya Vijana 8 wenye ushawishi Tanzania

Alikiba, Samatta Watajwa Kwenye Orodha ya Vijana 8 wenye ushawishi Tanzania
Mtandao unaohusika na tafiti mbalimbali zinazowahusu vijana wa Afrika kutoka nchini Ghana, 'Africa Youth Awards' umeweza kutoa orodha ya majina ya vijana 100 wenye ushawishi mkubwa kutoka kwenye nchi 26 za barani Afrika, kwa mwaka 2018.


Katika orodha hiyo ambayo imetolewa leo Septemba 04, 2018, Tanzania imeingiza takribani vijana nane ambao ni Ali Kiba, Falaja Nyalandu, Herieth Paul, Jennifer Bash, Jumanne Mtambalike, Mbwana Samatta, Millard Ayo, pamoja na Yusuf Bakhresa.

Vigezo ambavyo vimetumika ni pamoja na umri wa miaka 30 kushuka chini, kuwa na uwezo wa kuishawishi jamii ambapo haijahusisha kiwango cha mtu cha elimu.

Tuzo hizo za vijana wenye ushawishi mkubwa barani Afrika kwa mara ya kwanza zilizinduliwa mnamo mwaka 2016, ambapo zenyewe zimekuwa zikijikita zaidi katika kuwaangalia shughuli wanazozifanya vijana, ambazo kwa namna moja ama nyingine zimeweza kutoa mchango mkubwa kwa jamii inayomzunguka.

Orodha kamili soma hapa chini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad