Aliyemtukana Naibu Spika Kwenye Facebook Adakwa na Polisi


Aliyemtukana Naibu Spika Kwenye Facebook Adakwa na Polisi
Michael Simon Mwamwimbe mkazi wa Kiwira, Rungwe mkoani Mbeya anashikiliwa na Polisi akituhumiwa 'kumtusi' Naibu Spika kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Facebook

Mtuhumiwa anadaiwa kukiuka kifungu cha 18(1),(2) cha sheria ya makosa ya mtandaoni namba 14 ya mwaka 2015 kinachokataza kumtusi mtu kwa kuangalia rangi, uraia, dini ama asili yake

Aliandika hoja yenye kichwa "TUMECHOKA NA MBIO MBIO ZA TULIA ACKSON NA VING'ORA VYAKE"

Katika hoja hiyo alisema kuwa "Dkt. Tulia ni Mbunge wa Dar lakini kwao ni Tukuyu, Wilayani Rungwe......akija kutusalimia Wanyakyusa wenzake inakuaje apite kwa mbwembwe kama vile Polisi kibao na Spidi 120"

Aliongeza kuwa Mbunge wa Jimbo la Rungwe S. H. Amon akipita barabarani huwa anapita kimyakimya na kupungia Wananchi mkono
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad