John Soko(25) alisababisha vifo hivyo baada ya gari lake aina ya Toyota Brevis lenye namba za usajili T920 DGH kupinduka katika kijiji cha Ligunga, Tunduru mkoani Ruvuma
Kamanda wa Polisi, Jemen Mushy alisema jana kuwa baada ya tukio hilo kutokea hapo juzi Askari huyo wa Kikosi kimoja Jijini Arusha alikimbia na kutokomea kusikojulikana
Aliongeza kuwa Askari huyo alikuwa akitokea katika Hospitali ya Misheni ya Kiuma kuchukua mwili wa marehemu Msusa Mtetechi baada ya kuombwa na wanafamilia
Aidha, waliopoteza maisha ni Issa Mtonyole(51), Fatuma Abeid(70) na kaka wa dereva aliyetambulika kwa jina la Mbalale Hassan(31)